NCIC kuwakamata wanaoeneza chuki

Baada ya kushutumiwa kwa madai ya kushindwa kuthibiti matamshi ya chuki , tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa a��NCIC sasa imenoa makali kwa kuagiza kukamatwa kwa wanasiasa wanaoeneza chuki. Duru zinaarifu kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaotafutwa ili kuhojiwaA� kwa madai ya uchochezi ni mbunge wa Mt.Elgon John Serut na mpinzani wake Fredrick Chesebe Kapondi. Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya tume hiyo jijini Nairobi, mwenyekiti wa tume hiyo Francis Ole Kaparo amesema tume hiyo itamchukulia hatua bila uwoga au mapendeleo yeyote atakayepatikana akiwachochea wananchi .

Kuhusu mitandao ya kijamii, Kaparo alisema kuwa tume hiyo imetambua akuanti 176 za mitandao ya kijamii zinazotumika kueneza chuki .

Kaparo pia amevionya vituo fulani vya redio vinavyotangaza katika lugha za kiasili dhidi ya kueneza jumbe zinazoweza kuibua uhasama kabla ya uchaguzi mkuu ujao.