NASA yashutumu shambulizi la mwandishi mashuhuri Kuki Gallman

Muungano wa NASA umeshutumu shambulizi dhidi ya mwanamazingira na mwandishi Kuki GallmanA� na wafugajiA� katika shamba lake huko Laikipia. Kwenye taarifa,kinara mwenza wa muungano huo Raila OdingaA� ameshutumu kile ametaja kuwa uhuni, na kuihimiza serikali kuchukua hatua dhidi ya waliohusika . Kiongozi huyo wa upinzani amesema ni jambo la kusikitisha kwamba wamiliki wa hifadhi wanalengwa huko Laikipia, akisema serikali ina jukumu la kuwalinda.Matamshi yake yamejiri baada ya mumiliki wa hifadhi ya Gallmann Africa huko Laikipia kupigwa risasi na kujeruhiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji. Gallman ambaye alipata majeraha ya risasi tumboni, amesafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu. Hivi majuzi mumiliki hifadhi ya Sosian kwenye kauntiA� hiyoTristan Voorspuy, raia wa UingerezaA� aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.