NASA yapuuzilia mbali matakwa ya Jubilee ya kutaka kura za usais zihesabiwe tena

Muungano wa NASA umepuuzilia mbali majaribio ya chama cha Jubilee ya kutaka kura za uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita zihesabiwe tena badala ya marudio ya uchaguzi huo. Wakiongea jijini Nairobi, vinara wa upinzani Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula walisema kuwa uamuzi wa mahakama ya juu wa kufutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta ulikuwa wa mwisho na hauwezi kupingwa. Walikuwa wakiongea kwenye ibada ya kanisa la PAG huko Kabete ambako walikariri msimamo wao kwamba hakutakuwa na uchaguzi tarehe 26 mwezi ujao iwapo tume ya IEBC haitafanyiwa marekebisho. Wapinzani waliwaelezea wakenya ni kwa nini wanashinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu wa tume ya IEBC Ezra Chiloba pamoja na kupatikana kwa teknolojia mpya ya uwasilishaji matokeo kabla ya marudio ya uchaguuzi huo.