NASA yalenga Nakuru na kuhimiza amani wakati wa uchaguzi mkuu

Vinara wa muungano wa NASA walifanya kampeini zao katika kaunti yaA� Nakuru huku wakitoa wito kwa serikali kudumisha usalama ili kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu ujao unafanyika katika mazingira ya amani. Mgombea urais wa NASA, Raila Odinga alitoa wito kwa tume ya uchaguzi nchini kuandaa uchaguzi huru ulio wa haki. Vinara wenza wa muungano huo Mosses WetangulaA� na Musalia Mudavadi waliwahimiza wafuasi wao huko Kajiado, Uasin Gishu na Nakuru kutohamia maeneo mengine nchini wakati na baada ya uchaguzi wakisema usalama utaimarishwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu.