NASA yakanusha uwezekano wowote wa kufanya kikao na IEBC

Viongozi wa muungano wa upinzani-(NASA), wamekanusha uwezekano wowote wa kufanya kikao na maafisa wa tume ya (IEBC) hadi kutimizwa kwa matakwa yao. Wamesema (IEBC), bado haijatoa jawabu lolote kwa baruaA� yao na hivyo hawatashiriki mazungumzo yoyote na tume hiyo. Miongoni mwa matakwa ya-NASA ni kuharamishwa kwa kampuni ya Ufaransa a�?OT-Morphoa�?, ambayo wanadai ilitoa hongo hata kupewa kandarasi ya kupeperusha matokeo ya kura za Urais, na hivyo inapaswa kubebeshwa dhamana kutokana na visa vingi vya udanganyifu kuhusiana na uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Augosti. NASA inadai afisa mmoja wa IEBC, na mwingine mwandamizi wa serikali wanahusika na sakata hiyo. A�Kulingana na kinara wa NASA, Raila Odinga, pesa hizo za hongo zilitolewa kupitia kwa kampuni moja ya mawakili hapa Jijini Nairobi na kuwasilishwa kwa afisa huyo wa serikali ya kitaifa hatua kwa hatua. Aidha, Raila amedai kwamba kampuni hiyo ya teknolojia ya habari ilishirikiliana na kampuni mbili za mawasiliano ya simu katika wizi wa kura za Urais.A� Upinzani ambao tayari umeitaka serikali ya Ufaransa kuchunguza uhalifu huo wa maafisa wawili wa kampuni ya Morpho umekariri kwamba kampuni hiyo haiwezi kushirikishwa tena kwa kupeperusha matokeo ya kura za Urais. Aidha, upinzani unasisitiza kwamba maafisa waA� IEBC waliohusishwa na wizi wa kura sharti wafikishwe mahakamani, na kwamba muungano wa NASA utashiriki tuA� kwenye marudio ya uchaguzi wa Urais pindi tume hiyo ya IEBC chini ya uongozi wa Wafula Chebukati itakapotekeleza marekebisho ili kuhakikisha usawa kwa wagombeaji wote tarehe 17 Oktoba. Kwa upande wake kampuni ya OT Morpho, imekanusha madai ya kujihusisha na uovu wowote na imetishia kuwashtaki viongozi hao wa upinzani.