NASA kufanya kampeini zake Jijini Nairobi

Mbombeaji Urais wa muungano wa NASA, Raila Odinga leo ataongoza kampeini za muungano huo Jijini Nairobi ambazo kilele chake kitakuwa katika uwanja waA� Kamukunji huko Kibra. Raila anatarajiwa kuwaeleza wakaazi kile ambacho utawala wa NASA utawafanyia mara tu akishika hatamu za uongoziA� baada ya marudio ya uchaguzi wa Urais tarehe 17 Oktoba mwezi ujao. Odinga anatarajiwa pia kutoa jawabu lake kuhusiana na matamshi ya Rais eti huenda akaondolewa afisini iwapo atashinda katika marudio ya uchaguzi huo wa Urais ikizingatiwa kwamba muungano wa NASA hauna wajumbe wa kutosha katika ma-bunge yote mawili. Eneo la Kibra linachukulwia kuwa ngome ya NASA, na kiongozi huyo wa NASA aliwahi kuhudumu kwa muda mrefu kama mbunge wa eneo la Langa��ata ambalo linajumuisha eneo hilo la Kibera.