NASA wataka matokeo ya uchaguzi wa Urais kubatilishwa

Mawakili wa muungano wa NASA wanaitaka mahakama ya juu nchini kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi agosti kuambatana na rufaa waliowasilisha kwa msajili mkuu ambayo inaonesha makosa kwenye fomu za 34B katika maeneo bunge 90, ambazo miongoni mwa dosari nyingine hazikuwa na nembo za usalama. Akiwasilisha ripoti hiyo kwa msajili mkuu A�wa mahakama hiyo Anne Amadi, wakili James Orengo aliitaka mahakama hiyo kuzidurusu fomu za 34A na 34B huku akidai kuwa dosari zilizomo ziliathiri takriban kura milioni 5. Tume huru ya mipaka na A�uchaguzi kupitia wakili wake Paul Muite ilitaka rufaa hiyo ifutiliwe mbali.Jopo la majaji saba linatarajiwa kufanya uamuzi husu kesi hiyo tarehe mosi mwezi Septemba.

A�