NASA kuwasilisha waraka kwa IEBC kuhusu malalamishi ya upinzani

Muungano wa kitaifa wa upinzani (NASA) umewasilisha waraka kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuhusu malalamishi ya upinzani kuhusu shughuli ya uchaguzi.Muungano huo wa NASA ukiongozwa na kiongozi waA� CORD Raila Odinga uliikabidhi tume hiyo ya IEBC waraka huo jana wakati wa mkutano wa mashauriano na makamishna wa tume ya IEBC.Odinga aliwaambia makamishna hao kwamba upinzani unataka masuala yote ambayo huenda yakaathiri hadhi ya uchaguzi huo mkuu yashughulikiwe.Mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati aliuhakikishia upinzani na wakenya kwa jumla kwamba uchaguzi mkuu ujao utakuwa huru na wa haki lakini akavitaka vyama vya upinzaini viepuke kutoa matamshi yasiyokuwa na msingi kuhusu shughuli ya uchguziA� wakati vinapoandaa mikutano ya hadhara.Mkutano huo uliandaliwa kufuatia ombi la upinzani baada ya malalamishi kadhaa kuwasilishwa kuhusu nambari kadhaa za vitambulisho vya kitaifa zinazofanana.Tume ya IEBC ilichapisha majina ya watu elfuA� 78 ambao wamesajiliwa kwa nambari za vitambulisho zinazofanana au nambari za vitambulisho zisizokuwepo.