NASA kurejelea maadamano ili kushinikiza uchaguzi upya

Mrengo wa NASA unatarajiwa kurejelea maandamano ya umma mnamo ijumaa kushinikiza kuandaliwa kwa uchaguzi mpya wa urais. Barua iliyoandaliwa na wakili, Edwin Sifuna imesema mrengo huo umemfahamisha kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi, Japheth Koome kuhusu maandamano hayo jijni Nairobi.Muungano huo unasema maandamano hayo yatakuwa ya amani na ni sehemu ya juhudi zake kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi.Kwenye barua hiyo Sifuna amewataka polisi kuwapa ulinzi waandamanaji . Mwezi uliopita kaimu waziri wa usalama wa taifa Fred Matianga��I aliharamisha maandamano kati kati ya miji ya Nairobi,Mombasa na Kisumu. Hatua hiyo ilifwatia uporaji na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya awali ya muungano huo. Hata hivyo agizo hilo la Matianga��I lilibatilishwa na mahakama kuu.