Mshauri wa Raila asema ushindi wa Uhuru bado ni haramu

Mshauri wa kiongozi wa muungano wa upinzani wa (NASA), Raila Odinga, Salim Lone, amesema kwamba maoni ya muungano huo juu ya utawala wa Jubilee kama uliobuniwa kwa njia zisizo halali, hayajabadilika licha ya uamuzi wa mahakama ya juu wa kudumisha ushindi wa Rais A�Uhuru Kenyatta katika marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 26 Oktoba. Alisema kulingana na muungano wa NASA, uamuzi huo wa mahakama ya juu sio jambo geni, akidai kwamba uamuzi huo uliafikiwa chini ya shuruti. Lone alisema muungano wa NASA hautalaumu mahakama ya juu, bali unaihurumia. Muungano wa NASA haukushiriki kwenye marudio ya uchaguzi huo wala kuwasilisha rufaa ya kupinga matokeo yake