Nancy Macharia alaumu wizara ya fedha

Tume ya kuwaajiri waalimu-TSC inalaumu wizara ya fedha kwa uhaba wa waalimu hapa nchini. Afisa mkuu wa tume ya TSC, Nancy Macharia, amelaumu wizara ya fedha kwa kukosa kutoa fedha za kuwaajiri waalimu elfu-20 zaidi licha ya tume hiyo kutoa ahadi ya kuwaajiri waalimu katika shule za umma. Alipowasilisha mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu elimu, Bi. Macharia aliiambia kamati hiyo kwamba shule za msingi pekee zina uhaba wa waalimu 40,972, ilhali shule za sekondari zinahitaji waalimu 63,849 zaidi. Aliongeza kusema kwamba shule za sekondari ambazo zina mpito wa asilimia 100 zina uhaba wa waalimu 50,789. Nchi hii inakabiliana na uhaba wa waalimu ambao huenda ukaathiri masomo ya wanafunzi katika shule za msingi na upili. Afisa mkuu huyo wa tume ya TSC alisema wizara ya fedha ingali haijatia shilingi bilioni tano za kuwaajiri waalimu 12,696 zaidi tayari kwa mpito wa asilimia 100 kutoka shule za msingi hadi sekondari na shilingi nyingine bilioni 16 za kuwaajiri wanagenzi elfu-68 waA�A�taaluma ya ualimu