Nakumatt na Zoo Kericho kusalia kwenye ligi ya Sportpesa hadi kesi kuamuliwa

Timu za Nakumatt na ZOO Kericho zitasalia katika ligi kuu ya Sportpesa hadi kesi inayopinga kuondolewa kwao kwenyeA� ligi hiyo, itakaposkizwa na kuamuliwa na Mahakama ya rufaa, katika uamuzi wake kuhusiana na rufaa iliyowasilishwa na FKF, imethibitisha kuwa timu hizo mbili zitaendelea kushiriki katika ligi kuu humu nchini, hadi kesi inayopinga mfumo wa ligi hiyo itakapoamuliwa. Shirikisho la FKF lilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu, ulioagiza ligi kuu irejelee mfumo wa timu 16, badala yaA� timu 18, kulingana na uamuzi wa jopo la kusuluhisha mizozo ya kimichezo nchini mapema mwaka huu. HukuA� shirikisho la FKF likipendekezaA� mfumo wa timu 18, kampuni inayosimamia ligi kuu, KPL, inaupigia upatoA� mfumo wa timu 16