Naibu wa Mkurugenzi wa shirika la kuwasaidia watoto, UNICEF ajiuzulu

Aliyekuwa naibu wa mkurugenzi   wa shirika la kuwasaidia watoto la Umoja wa mataifa-UNICEF Justin Forsyth amejiuzulu cheo chake na kusema hangependa makosa yake ya zamani kutia doa hadhi ya shirika hilo.Forsyth alikabiliwa na  malalamishi matatu kuhusu tabia isiofaa dhidi ya wasichana,kabla ya kung’atuka kutoka kwa shirika hilo.Alishitakiwa kwa kuwatumia wasichana arafa za mapenzi na kugusia kuhusu mavazi yao.Forsyth aliomba msamama kuhusu jambo hilo kabla ya kuwasilisha waraka wa kujiuzulu kutoka shirika hilo.