Naibu gavana kaunti ya Nyeri kuapishwa leo alasiri

Naibu wa gavana wa kaunti ya Nyeri , Mutahi Kahiga, ataapishwa kuwa gavana wa nne wa kaunti hiyo leo alaasiri kufuatia kifo cha gavana marehemu Dkt. A�Wahome Gakuru, kilichotokea kufuatia ajali mbaya ya barabarani wiki iliyopita. Matayarisho ya sherehe hiyo yamekamilika katika afisi za serikali ya kaunti hiyo. Magavana kadhaa na maseneta wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa. Kuapishwa kwa Kahiga kuwa gavana wa kaunti ya Nyeri kutamaliza hali ya sintofahamu kuhusu kutwaa kwake kwa wadhifa huo kufuatia ripoti kwamba baadhi ya viongozi wanajaribu kumzuia kutwaa wadhifa huo. Wakati huo huo wahubiri huko Nyeri leo asubuhi A�waliitakasa afisi ya gavana wa kaunti ya Nyeri A�kabla ya sherehe ya kumuapisha gavana wa nne wa kaunti hiyo.Wahubiri hao walisema wanamuomba mwenyezi Mungu aondoe mapepo ya vifo ambayo yamewapokonya wakazi wa kaunti hiyo magavana wawili katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja.Wahubiri hao vile vile waliombea maendeleo na ufanisi kupatikana katika kaunti ya Nyeri.