Naibu Rais Ruto Atoa Wito Kudumishwa Kwa Umoja Nchini

Naibu rais William Ruto ametoa wito wa kudumishwa kwa umoja nchini huku akiwataka wakenya kupuzilia mbali siasa duni ambazo huenda zikazua mgawanyiko mkubwa nchini.Aliwashauri wakenya wa tabaka mbali mbali kuwa na mshikamano ambao watajivunia. Akihutubia wananchi katika soko la Wangige kaunti ya Kiambu,naibu rais alisema ni jambo la kuhuzunisha kwamba kwa zaidi ya miongo miwili sasa,siasa nchini zimechochewa na maslahi ya kikabila akiongeza kuwa serikali ya Jubilee imejitolea kuangamiza mgiwanyiko yote ya kijamii na kidini iliyoko nchini. Wakati huo huo,naibu rais amesema serikali inatekeleza mipango makusus ya kuimarisha hali ya maisha ya wakenya.
Awali naibu rais alijiunga na waumini wengine kwa ibada ya jumapili katika kanisa la PCEA Uthiru, kaunti ya Kiambu na kutoa wito kwa viongozi wa kidini kuombea umoja humu nchini.