Naibu Mwenyekiti Wa Nock Akamatwa

Naibu mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki nchini,NOCK, Ben Ekumbo A�amekamatwa na maafisa wa kitengo cha CID waliovamia makazi yake jijini Nairobi na kunasa makatoni ya jezi za timu ya Kenya ziilizopaswa kutumiwa katika michezo ya Olimpiki iliyokamilika mwezi agosti mwaka huu nchini Brazil.Maafisa hao walimkamata Ekumbo ambaye pia alikuwa naibu wa mkuu wa ujumbe wa kikosi cha timu ya Kenya baada ya kuvamia nyumba yake na kumhoji kabla ya kuondoka na maketoni yaliyojaa jezi A�zikiwemo za wanariadha na waogeleaji. Ekumbo ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa uogeleaji nchini huenda akafikishwa mahakamani leo na kuwa afisa wa tano wa kamati hiyo ya Olimpiki nchini kukamatwa kuhusiana na uchunguzi unaoendelea kufuatia A�kuibuka kwa madai ya usimamizi mbaya wa kikosi cha kenya kilichoshiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki.Licha ya madai hayo Kenya iliafikia matokeo yake bora zaidi katika michezo hiyo ya Olimpiki baada ya kujizolea nishani sita za dhahabu,sita za fedha na moja ya shaba. Mkuu wa ujumbe wa timu hiyo Stephen Soi, ,naibu mwenyekiti wa A�kwanza Pius Ochieng na katibu mkuu Francis K. Paul waliachiliwa kwa dhamana baada ya kufikishwa mahakamni kuhusiana na madai ya usimamizi A�mbaya wa kikosi hicho cha Kenya jijini Rio.