Nahodha wa Tusker FC James Situma Afichua Atakacho Jivunia Katika Taaluma Yake

Nahodha wa Tusker FC  James Situma  anaamini kuwa kikosi hicho kina uwezo wa kunyakua taji ya ligi kuu ya Sportpesa msimu huu.

Situma amefichua  kuwa litakuwa  jambo la kujivunia  katika taaluma yake iwapo timu hiyo itanyakua taji hiyo ya ligi kuu akiwa nahodha.

Aidha , Situma ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Sofapaka  alitwikwa jukumu la unahodha na kocha mkuu Paul Nkata mwezi Januari baada ya  Jesse Were  kuondoka na kujiunga na vigogo wa Zambia ZESCO United.

Chini ya uongozi wake Tusker FC imeshindwa mara moja pekee katika mechi tisa na kwa sasa inashikilia nafasi ya pili ligini kwa alama 20 sawa na Mathare United inayoongoza msururu huo.