A�Nahodha Mpya Kuiongoza Naijeria dhidi ya Misri

Kiungo wa kati wa timu ya Chelsea John Obi Mikel ameteuliwa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Naijeria.

Mikel ambaye ndiye mchezaji aliyeichezea super eagles kwa mda mrefu katika kikosi cha sasa, baada ya kucheza mechi ya kwanza mwaka wa 2006, ataiongoza naijeria itakapojuana na Misri machi tarehe 25 kwenye dimba ya kufunzu barani afrika.

Amhed Musa aliyeteuliwa kama nahodha na kocha Sunday Olisey baada ya Kustaafu kwa Vincent Enyeama, alisema ni muhimu Mikel kuwa nahodha wa timu ya taifa kwa kuwa ana umaarifa wa kutosha.

Mikel sasa ameahidi kuwa kiongozi mwema na kuwashukuru wachezaji wenzake kwa nafasi waliompa.

Naijeria itachuana na Misri ugani Ahmadu Bello Stadium, Kaduma. Misri wanaongoza kundi lao kwa pointi 6, mbili mbele ya naijeria.