Mzungu Apatikana Na Hatia Ya Kuwaua Wamerikani Weusi

Mzungu mmoja mbaguzi amepatikana na hatia ya kuwauwa waMarekaniA�A� 9 weusi waliokuwa kanisani jimboni Carolina kusini nchini Marekani. Ilisemekana mauaji hayo yalitekelezwa kwa misingi ya kibaguzi. Jopo la majaji 12 lilichukua muda wa saa mbili kumpata na hatia Dylann Roof mwenye umri wa miaka 22 kuhusiana na makosa yote 33 yaliyomkabili, yakiwemo yale ya chuki. Mshtakiwa atajua hatima yake mwezi ujao ikiwa atahukumiwa kunyongwa. Shambulizi hilo lililotekelezwa mwaka wa 2015 kwenye kanisa moja la kiMethodisti la Emmanuel African Episcopal lilizua wasi wasi nchini Marekani. Aidha liliibua upya swala la uhusiano wa kijamii nchini Marekani.

Roof alikuwa amewaambia polisi kuwa alikuwa na nia ya kuanzisha vita vya kijamii na alipigwa picha akiwa ameshika bendera ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo kwa wengi ni alama ya chuki. Kisa hicho kilisababisha kuondolewa kwa bendera hiyo kutoka kwenye ikulu ndogo ya jimbo la Carolina Kusini ambako imekuwa ikipepea kwa muda wa miaka 50 iliyopita. Wakili wa upinzani David Bruck alikubali kuwa Roof alitekeleza mauaji hayo, japo alisema hakuonyesha dalili za kutaka kuuwa.