Mzozo waendelea kukumba NASA

 

Mizozo ya ndani inaendelea kukumba muungano wa upinzani NASA huku mwanasiasa, Miguna Miguna,akimshutumu mpanga mikakati wa NASA A�David Ndii na afisa mkuu wa NASA , Norman Magaya, kwa kushirikiana kisiri na makundi kutoka nje. Miguna anadai kwamba wawili hao wanatumiwa na watu kutoka nje ya muungano huo kuvuruga upinzani. Miguna,kwenye ujumbe kwa maafisa hao wawili wa NASA,anasema ana habari za kuaminika kwamba Magaya na Ndii wanajaribu kuvuruga shughuli za vuguvugu la National Resistance Movement.Vuguvugu hilo lilipigwa marufuku na serikali kwasababu za kiusalama.Miguna alifurushwa kutoka hapa nchini na kupelekwa Canada wiki mbili zilizopita kwa jukumu alilotekeleza katika kumuapisha kiongozi wa NASA Raila Odinga tarehe 30 mwezi januari. Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka,kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na wa Ford Kenya Moses Wetang’ula,hawakuhudhuria sherehe hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa Uhuru Park. Kutokuwepo kwao kulidhaniwa kuwa ishara ya kusambaratika kwa muungano wa NASA , madai ambayo vigogo wa muungano huo wamekanusha.