Mwinyi Kazungu

Majina kamili naitwa Mwinyi Kazungu Nyawa. Nilianza utangazaji mwaka 2006 katika shirika la utangazaji nchini KBC kama mtayarishaji wa vipindi na matangazo ya biashara katika kitengo cha ubunifu.

Mwaka 2008, nilipewa kazi ya kudumu kama mtayarishaji wa vipindi. Mwaka huohuo nikapata nafasi kutangaza kipindi 'KETAU Express'. 

Hivi sasa najivunia sana kufanya kipindi maarufu cha vijana, kinachoongoza nchini kwa jina 'Top Mashariki' kwenye Radio Taifa kila siku ya juma kuanzia saa nne hadi saa nane mchane. Pia kipindi hiki hukujia katika runinga ya KBC Channel 1 kila Ijumaa saa nne usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *