Mwenyekiti Wa Tume Ya IEBC Ahojiwa Na EACC

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC, Isaack Hassan anahojiwa na maafisa wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi-EACC kuhusiana na kashfa ya Chicken gate. Hassan alifika katika afisi za tume hiyo leo asubuhi muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Malindi ambako alisimamia uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi. Hassan ndiye afisa wa hivi punde kuhojiwa na tume hiyo kuhusu kashfa ya Chicken gateA� iliyofichuliwa baada ya maafisa wa kampuni moja ya uchapishaji nchini Uingereza kupatikana na hatia ya kuwahonga maafisa wa Kenya ili kupata zabuni. Mahakama moja mjiniA�London iliipata na hatia kampuni ya uchapishaji ya Smith and Ouzman kwa kuwahonga maafisa nchini Kenya na Mauritania kwa shilingi milioni-A� 59 ili kupata zabuni. Wiki iliyopita mshukiwa mkuu katika kashfa hiyo,A�Trevor Oyombra, kamishna wa IEBC Yusuf Nzibo, aliyekuwa afisa mkuu mwandamizi waA�IEBC James Oswago na aliyekuwa waziri wa kawi Davis Chirchir walihojiwa kwa muda wa saa kadhaa. Idara ya kukabiliana na kashfa nchini Uingereza ilikabidhi stakabadhi za madai hayo ya ulaji rushwa kwa mwanasheria mkuu mwezi januari.