Mwendwa Kukabidhiwa Ofisi Tarehe tatu Machi

Shughuli za kukabidhiA� ofisi kutoka kwa aliyekuwa kinara waA� wa shirikisho la soka humu nchini, Sam Nyamweya kwa mwenyekiti aliyeteuliwa hivi majuzi, Nick Mwendwa, sasa itafanywa tarehe tatu mwezi ujao, baada ya NyamweyaA� kuomba muda zaidi wa kujiandaa kufuatia mkutano baina yao.

Nick Mwendwa aliyechukua hatamu zaA� uongozi juma lililopita akiwahutubia wanahabari baada ya kukitana na Nyamweya katika makao makuu ya shirikisho hilo uwanjani Nyayo, alisemaA� katika muda wa siku mbili zijazo ataweka mikakati makhususi huku mkutano wa kamati kuu ya taifa ya shirikisho hilo ukipangwa kuandaliwaA� kesho.

NyamweyaA� aliunga mkono matamshi ya Mwendwa na kusema anahitaji muda ya kujiandaa kukabidhi mamlaka.

Mwendwa na kundi lake wamekumbwaA� na majukumu kwani Harambee Stars itakabiliana na Guinea Bissau kwenye mchuano wao wa tatu wa kufuzu kwa kipute chaA� kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka 2017, itakapochuana na Guinea Bissau mwezi ujao.

Maandalizi kabambe yataiwezesha Stars kuhuisha matumaini yao ya kufuzu kwa fainali hizo huku ikishikilia nafasi ya pili kutoka nyuma baada ya kushindwa mchuano mmoja na kutoka sare mmoja.