Mwaniaji Urais Wa Marekani Donald Trump Kuzuru Mexico

trump
Mwaniaji urais wa Marekani wa chama cha Republican Donald Trump, anatarajiwa kuzuru Mexico leo,saa chache kabla ya kutoa hotuba ya kubainishaA� hatua atakazochukua kudhibiti uhamiaji haramu.Kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Trump alisema kuwa anatarajia kukutana na rais wa Mexico Enrique Pena Nieto ,ambaye amewaalika kuzuru nchi hiyo pamoja na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton.

Trump anatarajiwa kuzuru Mexico kati ya sherehe ya kuchangisha pesa jimboni California na hotuba yake kuhusu uhamiaji haramu mjini Phoenix,jimboni Arizona leo usiku.Itakumbukwa kuwa Trump ameshutumu wahamiaji haramu kutoka Mexico kwenye kampeini zake za uchaguziA� na kuapa kujenga ukutaA� kati ya nchi hizo mbili ili kuwazuia wahamiaji haramu.

Awali rais Pena Nieto alimshutumu Trump kwa kuhujumu uhusiano baina ya nchi hizo mbiliA� na kulinganisha jazba yake na ile ya aliyekuwa kiongozi wa ki-imla wa Ujerumani Adolf Hitler.Kiongozi huyo wa Mexico alisema kuwa amewaalika wagombea urais hao wa Marekani kwa mazungumzo na kwamba anatarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na Trump baadaye leo.