Kiunjuri ataka upinzani uiunge mkono serikali

Waziri wa ugatuzi Mwangi Kiunjuri ametoa wito kwa upinzani uiunge mkono serikali ili iweze kuendelea kutekeleza miradi iliyowaahidi wakenya wakati wa kampeini. Kiunjuri ambaye alikuwa akiongea na wanahabari baada ya kutoa ratiba ya utaratibu wa magavana kuchukua mamlaka, hatahivyo alifurahia kwamba kiongozi wa upinzani Raila Odinga ana wafuasi wengiA� na kumhimiza ajiunge na serikali katika kuleta umoja nchini baada ya uchaguzi mkuu wa hivi punde.