Mwandani Wa Kaimu Rais Wa Brazil Michel Temer Ajiuzulu

Mwandani wa kaimu rais wa Brazil Michel Temer amejiuzulu kufuatia kashfa mpya ya kisiasa nchini humo. Waziri wa mipango Romero Juca alidaiwa kunaswa kwenye kamera akipanga njama ya kuvuruga uchunguzi kuhusu kesi kubwa zaidi ya ufisadi kuwaki kukumba taifa hilo. Kwenye kanda hizo zilizotolewa kwa wanahabari, Juca anaonekana akisema angeweza kusimamisha uchunguzi kuhusiana na madai ya ufisadi kwenye kampuni kubwa zaidi ya mafuta nchini humo Petrobras kwa kushawishi kunga��atuliwa mamlakani kwa rais Dilma Rousseff. A�Juca hata hivyo amesema matamshi yake yametafsiriwa visivyo. Rousseff alisema kanda hizo zinathihirisha wazi kuwa kunga��atuliwa kwake mamlakani kupitia hatua ya bunge kulikuwa mapinduzi ya kisiasa yaliyopangwa na maafisa wakuu waliohusishwa na ufisadi katika kampuni ya Petrobas.