Mwanawe Trump akiri kukutana na wakili mmoja kutoka Urusi

Mwanawe rais wa MarekaniA� Donald Trump amekiri kukutana na wakili mmoja kutoka Urusi mwaka uliopita ambaye anasema alikuwa ameahidi kutoa habari zisizo za kuridhisha dhidi ya Hillary Clinton, lakini mwanawe Trump amesema kuwa Natalia Veselnitskaya hakumpa habari zozote muhimu kuhusiana na mwaniaji huyo wa urais.A� Kadhalika mkwewe rais Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni za Trump, Paul Manafort walikuwa kwenye mkutano huo ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye gazeti la New York Times. Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani. Mkutano huo na Veselnitskaya, unaosemekana kuwa na uhusiano na makao makuu ya serikali ya Urusi ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka uliopita kwenye jumba la Trump jijini New York majuma mawili baada yaA� Donald Trump kuteuliwa kuwa mwaniaji urais wa chama cha Republican. Shirika la kijasusi la FBI na bunge la Congress zinachunguza madai kwamba maafisa wa kampeni za Trump walishirikiana na makao hayo makuu ya serikali ya Urusi kudhalilisha kampeni za Clinton. Uchunguzi huo bado haujabainisha iwapo ushirikiano kama huo ulikuwepo.