Mwanawe rais Donald Trump kufika mbele ya baraza la Senate

Mwanaye wa kwanza wa kiume wa rais wa Marekani, Donald Trump, mkaza mwanaye na aliyekuwa meneja wa kampeni za Trump wanatarajiwa kufika mbele ya baraza la Senate nchini Marekani kuhusiana na madai kuwa Russian ilishawishi matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka-2016. Donald Trump Jr, Jared Kushner na Paul Manafort watahojiwa kuhusu uhusiano wao na maafisa wa serikali ya Russia. Swala kuu ni mkutano baina yao na wakili mmoja wa Russia mwaka uliopita. Wakati huo huo, rais Trump amesema hangelimteua Jeff Sessions kuwa mwanasheria mkuu kama angelijua anaweza kujinasua kutoka uchunguzi huo. Rais Trump pia aligusia mazungumzo baina yake na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin wakati wa mkutano wa nchi-20 zilizostawi kiuchumi duniani akisema walikuwa wakijuliana hali tu. Wanachama wa Senate na bunge la waakilishi nchini Marekani pamoja na mshauri maalum wa idara ya sheria wanachunguza ikiwa Russia ilishawishi matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani ambapo Donald Trump aliibuka mshindi.