Mwanaspoti bora Kenya kutangazwa leo

Sherehe za makala ya 14  ya  tuzo za mwanaspoti  bora wa mwaka SOYA zitaandaliwa leo  katika ukumbi wa jumba la mikutano ya kimataifa KICC. Miongoni mwa wale wanaowania tuzo za mwanaspoti wa mwaka ni  mabingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 Helen Obiri na Elijah Manangoi. Obiri na  Manangoi walitangazwa wanariadha bora wa mwaka kwenye tuzo za chama cha Riadha Kenya hasa baada ya kukosa kunyakua tuzo za wanariadha bora wa mwaka wa shirikisho la riadha duniani IAAF. Aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Ghana  Stephen Appiah ni mgeni rasmi wa sherehe hizo.Appiah, ambaye alicheza vilabu mbali mbali vikiwemo  Juventus ya Italia na Fenarbahce ya Uturuki anafuatia baada ya mwanariadha maarufu wa Ethiopia  Haile Gebrselassie  kuhudhuria sherehe za  mwaka jana.  Mwanaspoti bora wa mwaka atatia kibindoni shilingi milioni moja huku wakishindi katika viwango tofauti ya tuzo hizo wakipokea shilingi nusu milioni kila moja. Aliyekuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita 10,000  na 5,000  Vivian Cheruiyot  alinyakua tuzo ya mwanaspoti bora wa mwaka 2016.