Mwanasoka maarufu George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

Aliyekuwa mwanasoka maarufu George Weah amechaguliwa kuwa Rais wa Liberia huku kura zote kwenye marudio ya uchaguzi wa urais zikiwa zimehesabiwa. Weah amempiku mpinzani wake Joseph Boakari kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura. Habari kuhusu ushindi wa Weah zilipotangazwa, wafuasi wake walianza kusherehekea katika mji mkuu wa Monrovia. Atamrithi Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza barani Afrika kuchaguliwa kuwa Rais kwenye mpito wa kwanza wa kidemokrasia nchini Liberia baada ya miongo kadhaa. Weah alikuwa mwanasoka maarufu katika timu za ligi ya Uingereza za Paris St-Germain-PSG na AC Milan, kabla ya kukamilisha uchezaji soka huko Uingereza alipojiunga kwa muda mfupi na timu ya Chelsea na Manchester City.

Yeye ndiye mwanasoka wa pekee mwafrika kushinda tuzo ya kifahari ya mchezaji bora zaidi ya soka wa shirika la soka duniani FIFA na lile la Ballon Da��Or. Alijiunga na siasa baada ya kujiuzulu kandalanda mwaka wa 2002 na kwa sasa yeye ni seneta katika bunge la Liberia. Liberia taifa lililobuniwa na watumwa walioachiliwa nchini Marekani katika karne ya 19, halijakuwa na mpito shwari kutoka Rais mmoja aliyechaguliwa hadi kwa mwingine tangu mwaka wa 1944. Bi. Sirleaf alimshinda Weah kwenye marudio ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2005 na kuchukua hatamu za uongozi mwaka mmoja baadaye baada ya kukamilika vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe ambapo Rais Charles taylor alibanduliwa mamlakani na waasi.