Mwanariadha Jaroslav kupigwa marufuku katika mkahawa kwa kula chakula kingi

Mwanariadha wa Ujerumani, Jaroslav Bobrowski amepigwa marufuku kula katika mkahawa mmoja mnamouzwa chakula kingi kwa bei nafuu kwa madai kwamba anakula chakula kingi sana.

Bobrowski alisemekana kununua chakula cha gharama ya dola 18.49 lakini akala sahani mia moja za chakula. Mwenye mkahawa huyo alisema Bobrowski haruhusiwi kurejea humo tena kwa sababu alikula chakula kinachoweza kuwashibisha watu watano. Bobrowski hujinyima chakula kwa saa 20 na kisha anakula hadi atakaposhiba.