Mwanamume Azikwa Na Milioni 200 Nchini Uganda

Mwanamume wa umri wa miaka-52 nchini Uganda, Charles Obong amezikwa pamoja na zaidi ya shilingi milioni 200. Mwanamume huyo aliyefariki Disemba mwaka uliopita baada ya kuugua kwa muda mfupi alizikwa wakati wa sherehe za krismasi kwenye jeneza la chuma linalokisiwa kugharimu shilingi milioni-20. Imesemekana Obong aliyekuwa afisa wa ngazi za juu katika wizara ya utumishi wa umma aliweka akiba ya pesa hizo ili atumie kumhonga mungu siku ya hukumu ili asamehewe dhambi zake. Shemejiye David Elic amesema Obong aliacha wosia uliosema baada ya kifo chake, mkewe A�Margaret Obong anafaa kuweka pesa nyingi kwenye jeneza lake ili ampelekee mungu amsamehe dhambi zake.