Mwanamme Auawa Kwenye Ubalozi Wa Marekani,Nairobi

Mwanamume mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kumdunga kisu afisa wa kikosi cha GSU katika ubalozi wa Marekani ulio na ulinzi mkali huko Gigiri, jijini Nairobi. Kulingana na polisi, mwanamume huyo alipigwa risasi baada ya kumjeruhi afisa huyo kwa kumdunga kisu mkononi.A� A�Duru zinaarifu kwamba mwanamume huyo alikuwa akijaribu kuingia kwa nguvu katika ubalozi huo, alipozuiwa na afisa huyo langoni. Mwanajeshi huyo alipata majeraha ya kichwa na mkono kufuatia kisa hicho. A�Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani ilithibitisha kutokea kwa kisa hicho, ikiongeza kwamba hakuna afisa wa ubalozi huo aliyeathiriwa. Afisa huyo anaendelea kupata nafuu. Polisi wanachunguza iwapo mwanamume hiyo aliyekuwa na kisu alikuwa na washirika.