Mwanamke anayeshukiwa kuogoza genge la majambazi katika mitaa ya kifahari jijini Nairobi afikishwa mahakamani

Mwanamke anayeshukiwa kuongoza genge la majambazi ambao wamekuwa wakitekeleza A�wizi katika mitaa ya kifahari jijini Nairobi jana alifikishwa mahakamani. Lavender Akinyi Ogilo ambaye amekuwa wa kwanza kwenye orodha ya majambazi wanaotafutwa zaidi na maafisa wa usalama jijini Nairobi akiwa na washukiwa wengine wanne wamekabiliwa na mashtaka kadhaa kuhusiana na msururu wa visa vya wizi katika mitaa ya Muthaiga, Lavington naA� Kileleshwa. Mwanamke huyo alikamatwa baada ya polisi kuvamia nyumba yake mtaani Ruaka. Polisi walisema kuwa genge hilo linalojumuisha wanawake wawili na wanaume watoto limekuwa likiwakwepa maafisa wa usalama kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. A�Wakiongea walipofikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Milimani Francis Andayi, Ogilo na washirika wake walikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki-3 pesa taslimu kila mmoja.