Mwanahabari Phil Cox Aachiliwa Huru Na Sudan

Sudan imemwaachilia huru mwanahabari mmoja wa Uingereza ambaye alikamatwa na kuzuiliwa mwezi uliopita kwa kuingia nchini humo kinyume cha sheria. A�Kwa mujibu wa ubalozi wa Uingereza na vyombo habari nchini Sudan, mwanahabari huyo kwa jina Phil Cox alikabidhiwa kwa ubalozi wa Uingereza siku ya jumatano. Mipango inafanywa kumpeleka nchini Uingereza ili kumuunganisha na familia yake. Kuachiliwa huru kwake kunawadia baada ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza Boris Johnson na waziri wa Uingereza anayehusika na maswala ya Africa Tobias Ellwood kufanya A�mazungumzo na maafisa wa serikali ya Sudan. Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa mwanahabarin huyo alisamehewa na rais A�Omar al-Bashir.

A�