Mwana-Sarakasi Bill Cosby amehukumiwa miaka 3-10 kwa kosa la dhuma ya mapenzi

Jaji mmoja katika jimbo la Pennsylvania huko Marekani amemhukumu mwana-sarakasi Bill Cosby kifungo cha miaka mitatu hadi kumi baada ya kupatikana na makosa ya dhuluma za kimapenzi.

Cosby mwenye umri wa miaka- 81, ameagizwa pia kuhudhuria vikao vya ushauri millele na kuorodheshwa miongoni mwa watu hatari. Mwanasarakasi huyo alikataa kutamka lolote alipoulizwa kufanya hivyo. Wakati wa kesi dhidi yake mwezi April, Cosby alipatikana na hatia kutokana na mashtaka matatu ya kumdhulumu kimapenzi Andrea Constand mnamo mwaka 2004.

Cosby alijipatia umaarufu mnamo miaka ya 1980 nchini Marekani  kutokana na kipindi cha televisheni cha Cosby Show. Mnamo mwezi June mwaka 2017, afisa mmoja wa zamani wa chuo kikuu cha Temple  alisimulia jinsi Cosby, ambaye alimheshimu sana alipompatia dawa kabla ya kumdhulumu kima