Mwakilishi Wa Wadi Afikishwa Mahakamani Kwa Uchochezi

Mwakilishi wa wadi ya Makutani katika bunge la kaunti ya Baringo Reson Perkei alifikishwa mahakamani jana akishtakiwa kwa uchochezi.A� Perkei anadaiwa kuvuruga mkutano wa usalama ulioandaliwa mwishoni mwa wiki na naibu kameshina wa kaunti ndogo ya Marigat Felix Kisalu kushughulikia maswala ya usalama yanayojumuisha ongezeko la visa vya wizi wa mifugo katika sehemu hiyo.A� Inadaiwa kuwa mbunge huyo aliongoza ujumbe wa jamii ya Elchamus huko Marigat kwenda katika mkutano huo na kushutumu wazi afisi ya naibu kameshina wa kaunti hiyo ndogo kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu swala la wizi wa mifugo akidai kwamba hakuna mtu ambaye ametiwa nguvuni licha ya visa kadhaa vya uvamizi. Alidai kwamba uvamizi huo umesababisha vifo vya watu kadhaa huku wengine wengi wakiachwa bila makao. Alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mkazi wa Nakuru Liz Gicheha ambaye aliamua kwamba kesi hiyo ilikilizwe leo alasiri.