Mvutano Wa Kisiasa Wachacha Huko Kericho

Mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi na gavana wa Bomet Isaac Rutto wa chama cha Mashinani jana aliwaongoza wabunge wa Rift Valley walioasi kwenye kampeini ya kumpigia debe mgombezi wa chama cha Kanu wa kiti cha useneta wa Kericho Paul Sang iliyoandaliwa katika uwanja wa Kapkatet kaunty ya Kericho.

Viongozi hao ambao walikuwa ni pamoja na seneta Patrick Ole Ntutu waA� (Narok), John Lonyangapuo wa Pokot magharibi,seneta maalum Ziporah Kittony,mbunge wa Nandi Hill Alfred Keter , Johana Ngeno wa (Emurua Dikir) na Hellen Sambili wa (Mogotio) waliishutumu serikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwa eneo la Rift Valley.

Mbunge wa Emurua Dikkir Johana Ngeno aliikosoa serikali ya Jubilee kwa kukosa kutoa shilling millioni mia mbili ilizoahidi kwa ukarabati wa uwanja wa michezo wa Kapkatet.

Wakati wa mkutano huo wa hadhara, gavana wa Bomet Isaac Ruto aliishutumu serikali kwa kubagua kwenye uteuzi wa nyadhifa kuu serikalini na kutumia vibaya eneo la Rift Valley kujipatia kura.