Mvulana mmoja afariki Tana Delta kutokana na kipindupindu

Mvulana mmoja wa miaka kumi amefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika mji wa Garsen kaunti ndogo ya Tana Delta kufuatia mkurupuko wa ugonjwa huo juma hili.Watu wengine 14 wametibiwa katika kituo cha afya cha Garsen na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku wengine watatu wakilazwa.Afisa mkuu wa matibabu katika kaunti hiyo ndogo ya Tana Delta Dr. Nicholas Mwenda, alisema mvulana huyo alifariki katika mtaa wa Centre two mjini Garsen huku wengine wikiripotiwa kufariki kwenye vijiji kadha karibu na mji huo.Alisema maafisa wa afya wamekuwa wakiwahamasisha wakazi kuhusu haja ya kudumisha usafi na kusambaza dawa za kusafisha maji ya kunywa.Mikurupuko ya kipindi pindu ilianza kushuhudiwa katika eneo la Tana Delta tangu mwaka 2015 na takriban watu 20 wamefariki kutokana na maradhi hayo ya kuambukiza licha ya juhudi za kuhamasisha wakazi kuhusu umuhimu wa kudumisha usafi.