Mvua yaendelea kusababisha maafa nchini

Mvua inaendelea kusababisha maafa kote nchini huku hofu ikitanda ya kuzuka kwa magonjwa yanayotokana na maji . Watoto watatu ndio wa hivi punde kufariki katika kaunti ya Kilifi huku zaidi ya familia 250 zikiachwa bila makazi huko Magaribi baada ya mto Sabaki kuvunja kingo zake .Familia zaidi hapa nchini zinaendelea kushuhudia athari za mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Ziara ya shirika la msalaba mwekundu katika baadhi ya sehemu za eneo bunge la Magaribi kuitathmini kiwango cha uharibifu inaashiria uaharibifu mkubwa katika eneo hilo. Huko Sagana, iamesemekana gari lilitumbukia mto Sagana siku ya Jumamosi baada ya dereva wake kushindwa kulidhibiti. Halmashauri ya kiataifa ya uhifadhi wa mazingira NEMA imewashauri wakenya hasa wale wanaoishi karibu na mito kuhamia maeneo salama. Halmashauri hiyo imetahadharisha kuwa mito mingi mikubwa imejaa mchanga na matope na huenda ikavunja kingo zao. Waendeshaji magari pia wametakiwa kutahadhari barabarani.