Mvua inayonyesha jijini Nairobi yamulika Muundo msingi wa kuondoa maji taka

Muundo msingi wa kuondoa maji taka katika jiji la NairobiA�A�kwa mara nyingine umeangaziwa huku mvua inayoendelea kunyesha ikisababisha madhara. Mvua inayonyesha katika sehemu mbali mbali za nchi imejiri kama afueni kwa wengi hasa ikinyesha wakati ambapo kumekuwa na habari kuhusu uhaba wa maji na athari za hali ya ukame. Hata hivyo watumiaji barabara walilazimika kukaa barabarani kwa saa nyingi kwenye misongamano ya magari jijini. Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema mvua inayonyesha kwa sasa haitadumu kwa muda mrefu huku hali ya kiangazi ikitarajiwa baada ya juma lijalo kabla ya kurejelea msimu wa mvua ya masika.