Muungano wa NASA yahirisha kuapisha Raila kama rais

Muungano wa NASA kwa mara nyingine umeahirisha hatua ya  kutaka kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa rais.Wanachama wa kamati andalizi ambao walikuwa wameahidi  kutoa tangazo hilo jana,walikutana  katika makao makuu ya muungano huo ,kabla  kufichua  kuahirishwa kwa hafla hiyo hadi baadaye. Mwanasheria mkuu Githu Muigai tayari ametaja hafla hiyo kuwa uhaini ,lakini kiongozi wa NASA kwa upande mwengine anasema siku hiyo imetengwa kwa uzinduzi wa bunge la mwananchi.Na huku hayo yakijiri,baadhi ya makundi yanaendelea kutoa wito wa kuwepo kwa ukomavu wa kisiasa.Viongozi mbali mbali wa dini kwa mara nyingine wametoa wito wa kufanywa kwa mazungumuzo kati ya rais Uhuru Kenyatta  na kiongozi wa upinzani ili kutatua tofauti za kisiasa zilizopo,ambazo wamesema zinaweza kuzua machafuko hapa nchini zisiposhughulikiwa kwa uangalifu.