Muungano Wa Jubilee Washutumu Upinzani

Muungano wa Jubilee umeshtumu upinzani kwa kuonyesha hali ya kutokuwa na uaminifu katika juhudi zinazoendelea za kuerekebisha tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. Akizungumza na KBC kwa njia ya simu kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Aden Duale alishangaa ni kwani muungano wa Cord sasa unadai kwamba wakilishi wawili kutoka kila upande watashauriana mwanzoni kwa majadiliano kabla ya mchakato rasmi kuanza kupitia taratibu za bunge.

Duale alisistiza kwamba walipokuwa katika ikulu ya Nairobi na Rais waliunga mkono swala la kubuniwa kwa wanachama 11 ambao watashauriana na weenzao wa mrengo wa Cord ili kuandaa hoja ambayo baadaye itawasilishwa katika mabunge yote mawili ili kuidhinishwa.

Mrengo wa Jubilee tayari umewateua wakilishi wake wakiongozwa na Seneta wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi na mwenzake wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen.