Muungano Wa CORD Wapokea Hatua Ya Jubilee Ya Kutaka Kutatua Mzozo Wa IEBC Kwa Furaha

Muungano wa CORD umefurahia hatua ya Rais Uhuru Kenyatta A�ya kutangaza kwamba kamati teule ya bunge itabuniwa kutatua mzozo kuhusu tume ya uchaguzi. A�Akiwahutubia waandishi wa habari katika ofisi za muungano huo katika ofisi za jumba la capitol hill kinara wa CORD Raila Odinga alisema bado kuna maswala yanayohitaji kutatuliwa na pande zote mbili kabla ya kujadili mwelekeo ufaao. Aidha Raila alisema amekuwa akiwasiliana na Rais tangu siku ya Jumatano kuhusu namna ya kutatua swala hilo. A�Muungano wa CORD umemteua seneta wa siaya James Orengo A�na mbunge wa Tongaren A�Eseli simiyu A�kukutana na wenzao wa Jubilee kutatua mzozo huo. Aidha aliongeza kwamba maswala hayo yatakapotatuliwa katika muda wa saa 24 zijazo mazungumzo rasmi kuhusu IEBC yanaweza kuanza.