Mutua Ataka Serikali Iwakamate Maafisa Walioidhinisha Jengo La Huruma

Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha mawakili hapa nchini, Erick Mutua ametoa wito kwa serikali ihakikishe kwamba maafisa wa serikali ya kaunti ya Nairobi walioidhinisha ujenzi wa jengo liliporomoka huko Huruma ambalo kufikia sasa limesababisha vifo vya zaidi ya watu-20, wamekamatwa. Akiongea wakati wa hafla ya kuchangisha pesa katika shule ya msingi ya Mboru, Erick Mutua alisema majengo ya aina hiyo yalijengwa kutokana na watu wafisadi ambao hawajali maisha ya wakenya wasiokuwa na hatia.A� Alisema wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua kali ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanayojengwa yanaafiki viwango vinavyohitajika. Mutua alipendekeza wanakandarasi na wahandisi waliosimamia ujenzi wa jumba hilo washtakiwe ili kuhakikisha uzingatiaji sheria katika sekta ya ujenzi.A�A�