Musiambo awaonya wananchi kutozuru maeneo hatari Baringo

Mshirikishi wa eneo la Rift Valley Wanyama Musiambo amewaonya wananchi dhidi ya kuzuru maeneo ambako oparesheni za kiusalama zinatekelezwaA� katika kaunti za Baringo na Laikipia. Musiambo alisema kuwa ni hatari kuzuru maeneo hayo ambayo kwa sasa yanadhibitiwa na maafisa wa usalamaA� wanaojumuisha vikosi vya ulinzi nchini, vikosi vya-GSU na maafisa huduma ya taifa ya polisi. Alisema kuwa raia na wanasiasa wanapaswa kuwaruhusu maafisa wa usalama waliotumwa katika maeneo husika kufanya kazi yao ya kukabiliana na wahalifu bila matatizo yao.

Waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery aliorodhesha maeneo 19 katika gazeti rasmi la serikali katika sehemu za Baringo kusini na Tiaty kuwa maeneo hatari na yanayoathirika. Miongoni mwa maeneo yaliyoorodheshwa ni pamoja na Arabal, Kiserian, Mochongoi, Rugus, Mukutani, Chebinyinyi, Komolion, Chepkalacha, Makutano na Paka. Mengine ni pamoja naA� Orus, Loiywat, Silale, Nando, Tangulbei, Chepkererat, Kipnai, Ng’oron na Amaya. Viongozi wa kisiasa wa Pokot mapema juma lililopita walitoa wito kwa serikali kusimamisha oparesheni hiyo ya usalama katika eneo laA� north rift ili kutoa nafasi ya kufanywa kwa mazungumzo.