Museveni: Iweje kuwe na uchaguzi mwaka ujao kabla hatujaangamiza Corona?

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa itakuwa makosa kuandaa uchaguzi wa urais nchini humo unaotarajiwa mapema mwaka ujao kabla ya kukabiliwa kwa chamko la virusi vya Corona, hii ikiwa ishara kuwa huenda uchaguzi huo ukacheleweshwa.

Matamshi hayo yanajiri huku Uganda ikiripoti idadi ndogo ya maambukizi ya virusi hivyo ambapo kufikia sasa ni visa 121 pekee vya maambukizi hayo vilivyoripotiwa nchini humo.

Ingawaje hakuna tarehe iliyotengwa kwa uchaguzi huo wa mwaka ujao,kwa kawaida huandaliwa mwezi februari.Museveni ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 1986, hajathibitisha iwapo atawania tena wadhifa huo au la,ingawaje chama chake cha National Resistance Movement (NRM) kimemuomba kupeperusha bendera yake kwenye uchaguzi huo.