Murkomen: Kuondolewa kwangu kutaimarisha ndoto zangu za kisiasa

Seneta wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amesema kuondolewa kwake kwenye wadhifa wa kiongozi wa wengi kutaimarisha zaidi ndoto zake za kisiasa.

Murkomen amewataka wafuasi wake kutokata tamaa kufuatia tukio hilo. Murkomen alikuwa akiongea leo asubuhi wakati wa kikao cha bunge la seneti baada ya spika Kenneth Lusaka kutoa ujumbe katika bunge la seneti kuwa alipokea mabadiliko hayo yaliyofanywa na chama cha Jubilee.

Spika alisema wadhifa wa Murkomen umekabidhiwa rasmi kwa seneta wa Pokot Magharibi Samuel Poghisio huku wadhifa wa kiranja wa walio wengi uliokuwa wa seneta wa Nakuru Susan Kihika ukikabidhiwa Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata.