Mumeo Mwanamuziki Chelele Akanusha Mashtaka Ya Kumuua Mkeo

Polisi wa utawala Erick Musila amekanusha madai ya kumuua mkewe ambaye ni mwanamuziki wa kikalenjin Chelele. Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka-29 alijibu mashtaka dhidi yake siku ya jumatano katika mahakama ya Naivasha ambako kesi hiyo ilihamishwa hadi Kericho kufuatia vitisho dhidi ya mshtakiwa. Musila, ambaye hakujibu mashtaka dhidi yake siku ya jumatatu, alipelekwa na maafisa wa polisi hadi katika gereza kuu la Naivasha. Wakili wake, Aggrey Simiyu siku ya jumatatu alisema kwamba mteja wake hayuko tayari kujibu mashtaka dhidi yake. Lakini upande wa mashtaka uliieleza mahakama kwamba ripoti kutoka hospitali ya kaunti ndogo ya Kericho inaonyesha anaweza kujibu mashtaka hayo. Ripoti hiyo ilisema kwamba mshukiwa yuko katika hali nzuri ya kiakili kujibu mashtaka dhidi yake. Simiyu aliitaka mahakama iwaagize maafisa wa polisi wanaochunguza kesi hiyo wakabidhi mshukiwa stakabadhi zake za kibinafsi walizochokua kutoka kwake. Alisema maafisa hao walichukua kadi tatu za ATM, kitambulisho na shilingi 6,200 pesa taslimu kutoka kwa Musila baada ya kumkamata. Jaji Christine Meoli aliutaka upande wa mahakama kuieleza mahakama iwapo stakabadhi hizo ni sehemu ya ushahidi, wkesi hiyo itakapotajwa tarehe 24 mwezi huu. Kesi hiyo itasikizwa tarehe 9 na 10 mwezi Mei.