Muganda Miya Ajiunga Na Klabu Ya Uingereza ya Standard Liege

Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Uganda, Farouk Miya amejiunga na klabu ya Standard de LiA?ge inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji. Klabu hiyo kwa sasa imo nambari nane kwenye ligi hiyo.Miya amekuwa akichezea klabu ya Vipers Sports Club.Taarifa za awali zilikuwa zimedokeza kwamba klabu hizo mbili zimekubaliani kitita cha 400, 000 dola za Kimarekani, wakati akiwa bado anacheza michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani nchini Rwanda mwezi uliopita.

Miya, 19, aliwafungia Uganda penalti na akasaidia ufungaji wa bao la pili mechi yao ya kwanza CHAN ambayo walitoka sare ya 2-2 na Mali.